Sakata ya SHA: Zaidi ya watu 20 kushtakiwa kwa wizi wa shilingi bilioni 12.7

Dismas Otuke
1 Min Read

Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP) imetangaza kuwafungulia mashtaka zaidi ya watu 20, wakiwemo wakurugenzi wa hospitali na afisa wa baraza la matabibu nchini, kwa kuhusika katika sakata ya wizi wa shilingi bilioni 12.7, kwa hospitali ambazo hazina leseni mtaani Eastleigh.

Yamkini hatua hiyo inafuatia ufichuzi wa Mhasibu Mkuu wa Serikali uliobaini wizi wa shilingi bilioni 12.7, zilizowasilishwa na hospitali ghushi kudai malipo ya matibabu kutoka kwa mamlaka ya Afya ya nchini SHA.

Malipo hayo yanadaiwa kutekelezwa baina ya Oktoba mwaka 2024 hadi Aprili mwaka 2025.

Tayari faili 1,188 zilitumwa kwa maafisa wa Polisi kwa uchunguzi tangu kuanza kwa SHA iliyotwaa nafasi ya bima ya NHIF mwaka uliopita.

TAGGED:
Share This Article