Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja ni miongoni mwa mashahidi watatu watakaokula kiapo kutoa ushahidi dhidi ya Naibu Rais Rigathi Gachagua.
Wengine watakaotoa ushahidi siku ya Jumanne katika bunge la kitaifa dhidi ya Gachagua ni Katibu wa Baraza la Mawaziri Mercy Wanjau, na aliyekuwa kaimu wa Afisa Mkuu mtendaji wa halmashauri ya dawa nchini KEMSA,Andrew Mulwa.
Bunge la kitaifa limetanga Jumanne hii Oktoba 8 kuwa siku ya kuskiza na kuamuliwa kwa mashtaka 11 yaliyowasilishwa dhidi ya Naibu Rais, kama sababu za kung’atuliwa afisini na Mbunge wa Kibwezi West Eckomas Mwengi Mutuse .
Mulwa anasema ana ushahidi wa Gachagua kushawishi zabuni ya vyandarua vya mbu mwaka 2023 vya thamani ya shilingi bilioni 3.7, alipokuwa afisini kama Afisa Mkuu mtendaji wa KEMSA.
Wanjau anasema kuwa ana ushahidi wa Gachagua kuwachochea watu kutohama maeneo yaliyo mita 30 karibu na mito katika kaunti ya Nairobi, kufuatia mafuruko yaliyosomba watu na nyumba na kusababisha vifo.
Gavana Sakaja pia atataoa ushahidi jinsi Gachagua alivyopinga na kuhitilafiana na usimamizi wa masoko ya kaunti ya Nairobi.