Sajili mpya za ardhi kubuniwa kuharakisha utoaji hatimiliki nchini, asema Kindiki

Martin Mwanje
1 Min Read

Serikali ya Kenya Kwanza itaharakisha utoaji wa hatimimiliki za ardhi kwa raia kote nchini. 

Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki amesema ili kuharakisha utoaji wa hatimiliki hizo, serikali itachapisha kwenye gazeti rasmi la serikali sajili mbili mpya za ardhi kote nchini.

Lengo ni kurahisisha upatikanaji wa huduma bora kwa raia.

Akizungumza leo Jumanne akiwa katika eneo la Chala Njukini, kaunti ya Taita Taveta, Prof. Kindiki amesema serikali itachapisha sajili mbili mpya za ardhi katika maeneo ya Taveta na Voi.

Akiwa eneo hilo, wakazi 1,301 wa eneo la Chala Njukini, eneo bunge la Taveta walipatiwa hatimiliki za ardhi.

Wakati huohuo, Naibu Rais amesema serikali itatoa kipaumbele kwa ukamilishaji wa miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa nchini.

Miradi hiyo inajumuisha barabra ya kilomita 66k ya Taveta-Njukini- Chala- Rombo -Ilasit Road inayounganisa kaunti za Taita Taveta na Kajiado.

Wabunge  John Bwire (Taveta), Haika Mizighi (Mwakilishi wa Wanawake, kaunti ya Taita Taveta), na Katibu katika Wizara ya Ardhi ,ixon Korir ni miongoni mwa waliokuwepo. waka

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *