Takriban wamiliki 100 wa biashara za maonyesho wamenufaika katika awamu ya pili ya mradi wa kuongeza tija za biashara kutoka kwa kampuni ya Safaricom maarufu kama ‘Grow with Safaricom Business’.
Kongamano hilo ambalo lilifanyika chini ya kaulimbiu ya “Kujenga chapa yenye nguvu kidijitali” lililenga kuwawezesha wajasiriamali kwa njia nne: kuwapa wateja uzoefu wa kipekee, kuwa na ufanisi katika utekelezaji, kuwaweka mbele katika uvumbuzi na mikakati ya ukuaji wa biashara.
Taasisi ya umma ya Kenya ya utafiti na uchanganuzi wa sera za Umma inakadiria kuwepo kwa zaidi ya biashara ndogo ndogo na za kadri milioni 7.4, zinazowaajiri takriban Wakenya milioni 14.9 katika sekta mbalimbali .
Wajasiriamali wadogo walipata fursa ya kubadilishana mawazo na mbinu za kibiashara wakati wa kongamano hilo na maarifa muhimu kuhusu jinsi ya kuendeleza ushindani katika nyakati hizi za kidijitali .
Awamu ya kwanza ya kongamano hilo iliyoandaliwa mwezi Machi ilinufaisha wajariamali 50 na sehemu ya vikao 12 vitakavyoandliliwa mwaka huu.