Imesalia saa chache tu, ambapo kinyang’anyiro cha kuwania Ikulu ya White House kimepamba moto – katika ngazi ya kitaifa na katika majimbo muhimu zaidi yanayoshindaniwa.
Zoezi la kupiga kura limekaribia,kukiwa na tofauti ndogo kati ya Donald Trump au Kamala Harris wakiweza kuwa na alama mbili au tatu kuwawezesha kushinda kwa urahisi.
Suala la kwa nini kila mmoja anaweza kufanya vizuri linapokuja suala kujiimarishia kambi ya wapiga kura katika maeneo sahihi,na kisha kuhakikisha kuwa kweli wanajitokeza.
Tuangazie kwanza uwezekano wa historia ya rais aliyeshindwa kuweza kuchaguliwa tena kwa mara ya kwanza katika miaka 130.
Trump anaweza kushinda kwa sababu zifuatazo
1.Kutokuwa madarakani
Uchumi ni kipaumbele kwa wapiga kura, na wakati ukosefu wa ajira ni mdogo na kupanda kwa soko la, Wamarekani wengi wanasema wanakabiliana na ongezeko la gharama za Maisha.
Mfumuko wa bei ulifikia viwango ambavyo havijawahi kushuhudiwa tangu miaka ya 1970 baada ya janga la Covid, ikimpa Trump nafasi ya kuhoji “Je, hali ni bora sasa kuliko miaka minne iliyopita?”
Mnamo 2024,wapigakura duniani kote wamevitupilia mbali vyama tawala kutokana na kupanda kwa gharama za maisha,baada ya janga la Covid.Wapigakura wa Marekani pia wana shauku ya mabadiliko.
Ni robo pekee ya wamarekani wanasema wanaridhishwa na uelekeo wa nchi huku theluthi mbili wakishindwa kuridhishwa na hali ya uchumi.
Harris amejaribu kuwa mgombea mpigania mabadiliko lakini kama makamo war ais amekuwa na kibarua kigumu cha kuonesha utofauti kati yake na Joe Biden ambaye hakuwa mgombea maarufu.
2. Hakabiliwi na shutuma nyingi
Licha ya msukosuko wa ghasia za Januari 6, 2021 katika Ikulu ya Marekani, mfululizo wa mashtaka na hatia ya jinai ambayo haijawahi kushuhudiwa, uungwaji mkono wa Trump umesalia thabiti kwa mwaka mzima kwa 40% au zaidi.
Wakati chama cha Democrats na wahafidhina wanaompinga Trump” wanasema hafai kushika wadhifa huo, Warepublican wengi wanamuunga mkono huku Trump akisema yeye ni mwathirika wa kisiasa.
Huku pande zote mbili zikiwa zimejizatiti, anahitaji tu kushinda kiasi cha kutosha cha wapiga kura ambao bado hawajaamua kura yao watampigia nani.
3. Maonyo yake juu ya uhamiaji haramu yanasikika
Kando na hali ya uchumi, uchaguzi mara nyingi huamuliwa na suala lenye mvuto wa kihisia.
Democrats wanaitegemea sera ya uavyaji mimba, huku Trump akiweka dau kwenye uhamiaji.
Baada ya makabiliano ya mpakani kuvuka viwango vya rekodi chini ya Biden,na idadi ya wahamiaji kuathiri majimbo ya mbali na mpaka,kura za maoni zinaonesha wapiga kura wanamuamini Zaidi Trump kuhusu Uhamiaji na kwamba anakubalika Zaidi Amerika kusini kuliko chaguzi zilizopita.
4. Wengi hawana shahada
Wito wa Trump kwa wapiga kura wanaojiskia kusahaulika na kuachwa
Nyuma, umebadilisha siasa za Marekani kwa kugeuza majimbo ya asili ya Democrats kama chama cha wafanyikazi kuwa Republican na kuimarisha ulinzi wa viwanda vya Marekani kwa kuwepo ushuru.
5. Anaonekana kama mtu mwenye nguvu katika ulimwengu usio na utulivu
Wapinzani wa Trump wanasema anadhoofisha miungano ya Marekani kwa kujihusisha na viongozi wa kimabavu.
Rais huyo wa zamani anaona kutotabirika kwake kama uimara wake, hata hivyo, anasema kwamba hakuna vita kubwa vilivyoanza alipokuwa katika Ikulu ya White House.
Wamarekani wengi wanakasirishwa kwa sababu tofauti,kama Marekani kutuma mabilioni ya pesa Ukraine na Israel na kufikiri Marekani ni dhaifu chini ya utawala wa Biden.
Wapiga kura waliowengi , hasa wanaume ambao Trump amekutana nao kupitia podikasti kama vile Joe Rogan, wanaona Trump kama kiongozi mwenye nguvu zaidi kuliko Harris.

Harris anaweza kushinda kwa sababu:
1. Yeye sio Trump
Licha ya kunufaika kwa uwepo wa Trump,anabaki kuwa mtu wa tofauti sana. Mnamo 2020, alishinda rekodi ya kura kwa mgombea wa Republican, lakini alishindwa kwa sababu Wamarekani milioni saba zaidi walijitokeza kumuunga mkono Biden.
Wakati huu, Harris anakabiliana na ujio wa Trump. Anamwita “fashisti” na tishio kwa demokrasia, huku akimnanga kwamba ataendeleza vituko na migogoro”.
Kura ya maoni ya Reuters mnamo mwezi mwezi Julai ilionyesha kuwa Wamarekani wanne kati ya watano wanahisi nchi hiyo inazidi kudorora.
Harris anataraji wapiga kura – haswa Republican wenye msimamo wa wastani watamuona kama mgombeaji mwenye utulivu.
2. Sio Biden
Democrats walikuwa na kila uelekeo wa kushindwa ambapo Biden alijiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho. Wakiwa wameungana kwa shauku ya kumshinda Trump, chama hicho kilimuunga mkono Harris haraka. Huku akiungwa mkono tangu alipotia nia, alitoa ujumbe wa kusonga mbele bele zaidi ambao ulisisimua.
Harris amepunguza baadhi ya zilizokuwa sera za Biden.
Mojawapo ni umri – kura za maoni mara kwa mara zilionesha kwamba wapiga kura walikuwa na wasiwasi juu ya Biden kufaa kushika nafasi ya urais.
Sasa kinyang’anyiro kimebadilika, na ni Trump ambaye anawania akiwa mzee zaidi kuwahi kushinda Ikulu ya White House.
3. Amepigania haki za wanawake
Huu ni uchaguzi wa kwanza wa rais tangu Mahakama ya Juu ya Marekani kubatilisha Roe v Wade na haki ya kikatiba ya kuavya mimba.
Wapiga kura wanaounga mkono kuhusu kulinda haki za uavyaji mimba kwa wingi walimuunga mkono Harris, na tumeona katika chaguzi zilizopita – haswa mihula ya kati ya 2022 – kwamba suala hilo linaweza kuchochea watu kujitokeza kupiga kura na kuathiri
Matokeo.
Wakati huu, majimbo 10, ikiwa ni pamoja na jimbo la swing Arizona, yatakuwa na mipango ya kupiga kura kuwauliza wapiga kura jinsi utoaji mimba unapaswa kudhibitiwa. Hii inaweza kuongeza uungwaji mkono kwa Harris.
Kihistoria pia azma yake ya kuwa rais wa kwanza mwanamke inaweza pia kuimarisha uongozi wake miongoni mwa wapiga kura wanawake.
4. Wapiga kura wake wanauwezekano mkubwa wa kujitokeza
Makundi ambayo Harris anauungwaji mkono mkubwa, kama wasomi wa chuo kikuu na wazee, wana uwezekano mkubwa wa kumpigia kura.
Democrats hufanya vyema zaidi na makundi ya watu wengi waliojitokeza, wakati Trump akipata mafanikio kwa makundi ya chini ya washiriki kama vile vijana na wale wasio na elimu ya chuo kikuu.
Trump, kwa mfano, anashikilia anaongoza miongoni mwa wale waliojiandikisha lakini hawakupiga kura mwaka wa 2020, kwa mujibu wa kura ya maoni ya New York Times/Siena.
Swali kuu, basi, ni ikiwa watajitokeza wakati huu.
5. Amechangisha fedha nyingi na kugharamika zaidi
Sio siri kuwa chaguzi za Mareknai ni ghali, na 2024 ni ghali zaidi kuwahi kutokea.
Lakini linapokuja suala la matumizi ya mamlaka- Harris yuko juu. Amepiga hatua zaidi zaidi tangu kuwa mgombea mnamo Julai akilinganishwa na Trump katika kipindi chote tangu Januari 2023, kwa mujibu wa uchambuzi wa hivi karibuni wa Financial Times, ambao pia ulibaini kuwa kampeni yake imegharimu karibu mara mbili zaidi ya gharama za matangazo.
Hii linaweza kufahamika kupitia kinyang’anyiro ambacho hatimaye kitaamuliwa na wapiga kura katika majimbo yanayolengwa kwa sasa na matangazo ya kisiasa.