Rwanda imetuma maombi ya kutaka kuandaa mashindano ya mbio za magari ya Formula one, maarufu kama Langalanga .
Haya yamethibitishwa na Rais wa Rwanda President Paul Kagame Ijumaa usiku.
Afisa Mkuu mtendaji wa Formula One Stefano Domenicali,ameahidi kulipa bara la Afrika maandalizi ya mkondo mmoja wa mashindano ya Grand Prix ya Formula one, huku akikiri mazungumzo kuendelea na nchi ya Rwanda kwa miezi kadhaa kwa sasa.
Endapo ombi lao litaidhinishwa, itakuwa mara ya pili kwa mashindano hayo kurejea Afrika, tangu Afrika Kusini iwe mwenyeji mwaka 1993 mjini Johanesberg.
Endapo F1 wataridhia ombi la Rwanda ,taifa hilo la Afrika mashariki litaandaa mashindano hayo katika barabara mpya ya kilomita 40, inakayojengwa karibu ya uwanja wa ndege wa Bugesera takriban kilomita 40 kutoka jiji kuu la Kigali.
Shurikisho la mashindano ya magari duniani linaandaa mikutano yake barani Afrika kwa mara ya kwanza nchini Rwanda .