Rais William Ruto amesema serikali yake imeongeza ufadhili kwa vyuo vikuu kutoka shilingi bilioni 45 hadi 82 kwa kila mwaka, tangu ashike hatamu za uongozi.
Ruto amesema hayo Jumapili jioni katika ukumbi wa KICC kwenye kikao cha kujadili mfumo mpya wa ufadhili wa vyuo vikuu nchini.
Rais amewahimiza wanafunzi wanaopokea mikopo ya masomo kuilipa mapema ili kuwaruhusu wengine kupata pia ufadhili.
Ruto amejibu maswali kadhaa kufafanua utata unaoghubika mfumo huo wa ufadhili.
Baadhi ya wanafunzi waliohudhuria kikao hicho wamehoji uwazi wa mfumo mpya wa ufadhili wakitaka ufutiliwe mbali.
Rais Ruto anasema mfumo huo unakusudia kuhakikisha wanafunzi kutoka familia maskini zaidi nchini wananufaika na ufadhili wa masomo kutoka kwa serikali.