Ruto:Hatutalazimisha vyama kujiunga na UDA

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto amesema kuwa chama chake cha United Democratic Alliance,hakitalazimisha vyama vingine kujiunga nacho.

Ruto ifichua haya siku ya Ijumaa katika ukumbi wa Bomas, alipoongoza mkutano wa viongozi wa kitaifa wa chama hicho .

Kauli hiyo inazima joto ambalo limekuwepo kuhusu njama ya UDA, kushurutisha kuvunjwa kwa vyama washirika kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Baadhi ya vyama vilivyo kwenye muungano huo ni; Ford Kenya chake Spika wa bunge la kitaifa Moses Wetangula,ANC cha waziri Musalia Mudavadi na Maendeleo Chap Chap cha waziri Alfred Mutua.

UDA wamepanga kuandaa uchaguzi wa viongozi wa mashinani Disemba mwaka huu kabla ya uchaguzi wa kitaifa.

Website |  + posts
Share This Article