Ruto: Uzalishaji wa chakula duniani unapaswa kufanyiwa mabadiliko

Martin Mwanje
1 Min Read

Rais William Ruto sasa anasema kuna haja kwa dunia kufanyia mabadiliko mifumo yake ya namna inavyozalisha na kuchakata chakula. 

Ruto amesisitiza umuhimu wa kutoa fedha za kuwasaidia wakulima wadogo wadogo katika hatua anayosema itahakikisha dunia ina chakula cha kutosha cha kukidhi mahitaji ya kila mtu.

“Umuhimu wa dharura kwa mabadiliko ya dunia juu ya namna tunavyozalisha, kuchakata, kusambaza na kutumia chakula ni suala linalopaswa kusistizwa zaidi,” alisema Rais Ruto wakati akihutubia Mkutano wa pili wa Viongozi Wakuu wa Kukadiria Mifumo ya Chakula wa Umoja wa Mataifa  (UNFSS+4) unaofanyika mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.

“Kwa misingi hii, tunapaswa kutoa fedha ambazo ni muhimu katika kuwasaidia wakulima wadogo wadogo, kampuni zinazochipukia, na wawekezaji katika kilimo na kuhamasisha suluhu bunifu za fedha za kidijitali kama vile M-PESA.”

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni, Rais wa Somali Hassan Mohamud na mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC) Mahmoud Ali Youssouf ni miongoni mwa waliokuwepo. 

Website |  + posts
Share This Article