Ruto: Sio mzaha, barabara ya Isiolo-Mandera itakamilishwa

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto

Rais William Ruto amethibitisha kuwa serikali imejitolea kukamilisha ujenzi wa barabara ya kilomita 750 ya Isiolo-Mandera, aliyoahidi alipozuru Kaskazini mwa Kenya mapema mwezi huu.

Akizungumza leo Jumatano, kiongozi wa taifa alisema ujenzi wa barabara ni mojawepo wa ajenda za utawala wake, kuhakikisha usawa wa maendeleo katika maeneo yote ya nchi, haswa maeneo ambayo kihistoria yametengwa kimaendeleo.

“Nilikuwa Kaskazini mwa Kenya na nilitangaza kutekelezwa kwa mradi mkubwa wa ujenzi wa barabara kutoka Isiolo kupitia Wajira hadi Mandera, na wengine wanafikiria ni mzaha,” alisema Rais Ruto.

“Nimejitolea kukamilisha ujenzi wa barabara ya kilomita 750 kutoka Isiolo hadi Mandera, kwa sababu kwa muda mrefu tumetelekeza eneo la Kaskazini mwa Kenya,” alingeza kiongozi huyo wa taifa.

Matamshi ya Rais yamejiri baada ya kukashifiwa katika mitandao ya kijamii huku ufahamu wake wa barabara na maeneo katika kaunti za Isiolo na Mandera ukilengwa.

Siku ya Jumanne, Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki, aliwafokea wakosoaji wa serikali akisema utawala wa Rais Ruto umeangazia kukamilisha miradi muhimu kwa wakati.

“Watu wanaweza kutukejeli, lakini tutatimiza. Mradi huu si mzaha, kazi inaendelea na itakamilishwa kabla ya uchaguzi wa mwaka 2027,” alisema Prof. Kindiki.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *