Ruto na Museveni wahudhuria tamasha la kitamaduni la Piny Luo, Siaya

Martin Mwanje
1 Min Read
Marais Yoweri Museveni, William Ruto na Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga wakati wa tamasha la Piny Luo, Siaya

Marais William Ruto na Yoweri Museveni wa Uganda wamehudhuria tamasha la kitamaduni la Piny Luo ambalo limekuwa likifanyika katika kaunti ya Siaya. 

Rais Museveni alilakiwa na mwenyeji wake punde baada ya kuwasili nchini mapema leo Alhamisi.

Ruto alikuwa ameandamana na Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga.

Kwenye hotuba yake, Rais Ruto aliwahimiza Wakenya kujivunia tamaduni na turathi za nchi yao.

Aidha, Ruto alitoa mchango wa shillingi millioni mia moja kwa jamii ya wavuvi katika eneo la Nyanza kama sehemu ya juhudi za kuunga mkono tamasha hizo.

Rais pia alifungua rasmi bewa la Chuo Kikuu cha Ramogi lililojengwa kwa gharama ya shilingi millioni 400 na kuagiza wanafunzi wa kwanza wajiunge nalo mwezi huu.

Nayo mito ya kuyaunganisha mataifa ya bara la Afrika ilipamba moto.

Ni mito iliyoungwa mkono na Rais Museveni na Raila anayewania uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, AUC.

Hususan, Raila alitoa wito kwa serikali za mataifa ya Afrika zichukue hatua za kuimarisha biashara baina yao namna yanavyofanya mabara mengine.

Pembezoni mwa tamasha hilo, viongozi hao walitarajia kuzungumzia namna ya kupunguza mafarakano ya mara kwa mara kati ya wavuvi wa Kenya na Uganda Ziwani Victoria.

 

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *