Ruto na Gachagua watakiwa kutatua mzozo baina yao

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto na Naibu wake Rigathi Gachagua.

Wabunge wawili wametoa wito kwa Rais William Ruto na Naibu wake Rigathi Gachagua, kutatua mzozo kati yao wakisema hali hiyo inaweza sababisha madhara makubwa na kuhujumu maendeleo ya nchi hii.

Wawili hao Caroli Omondi wa Suba Kusini na Elisha Odhiambo wa Gem, waliyasema hayo wakati wa mashindano ya nyimbo za kidini zilizofanyika katika kanisa la Central SDA, Kaunti ya Homa Bay.

Omondi aliwahimiza wananchi kuangazia ukuzaji wa uchumi wa taifa hili, akidokeza kuwa lengo hilo linaweza timizwa kupitia umoja na ushirikiano.

Aidha, Omondi alielezea imani kwamba suluhisho la kisiasa litapatikana iwapo viongozi hao wawili watashiriki meza ya mazungumzo.

Kwa upande, Odhiambo alimtaka naibu rais, kuwadhibiti washirika wake aliodai wanatoa cheche za maneno yanayoweza kuchochea migogoro zaidi hapa nchini.

Share This Article