Ruto: Mfumo wa elimu ya juu ulifanyiwa utafiti na kuidhinishwa na wataalam

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto ametetea mfumo mpya wa kufadhili elimu ya juu akisema kuwa  unaangazia zaidi uwezo wa kifedha kwa familia maskini.

Ruto amesema  haya Jumapili jioni alipoongoza kikao na wanafunzi wa vyuo vikuu katika ukumbi wa KICC  kuhusu mfumo huo wa kufadhili elimu.

Rais ameongeza kuwa wanafunzi yatima wanalipiwa karo kwa asilimia 95 huku wakijilipia asilimia tano pekee.

Amesifu mfumo huo akisema ndio bora kwa wanafunzi.

Hata hivyo, wanafunzi kadhaa wa vyuo vikuu wamelalamikia mfumo wakisema wamewekwa katika makundi yasiyostahiki ya ufadhili licha ya kutojiweza kifedha.

Huku wamekata rufaa dhidi ya uamuzi wa kuwaweka katika makundi hayo, baadhi wametaka mfumo mpya wa ufadhili ufutiliwe mbali kabisa.

 

Share This Article