Ruto: La muhimu sasa ni kutengeneza fursa za ajira kwa vijana

Marion Bosire
2 Min Read

Rais William Ruito amesema jambo la maana kwa sasa ni kuhakikisha fursa za ajira kwa vijana ambao ndio wengi katika idadi jumla ya watu ulimwenguni.

Akizungumza kwenye kongamano linaloendelea la vijana wa bara Afrika humu nchini, Rais Ruto alialika wanaohudhuria kongamano hilo, kuangazia uundaji wa fursa hizo.

Alitaja pia utambuzi wa thamani na utafutaji wa ufanisi huku akiwaomba wakabili changamoto za sasa kwa kutumia akili zao, ubunifu na uwezo katika uvumbuzi.

“Ninawaomba muwe mstari wa mbele katika kubadilisha bara Afrika, kuhakikisha sauti yenu inasikika, juhudi zenu zinahesabiwa na kuhakikishiwa kusika.

Kiongozi wa nchi alisema pia kwamba mabadiliko yanaendelea kushuhudiwa barani Afrika na anaamini kwamba tuko katika nyakati tofauti, Afrika mpya ambapo uvumbuzi utavuka mipaka, ubunifu ukue bila vikwazo na ndoto za bijana zitimie.

Kuhusu mabadiliko ya tabianchi, Rais Ruto alisema kwamba vijana lazima wawe mabingwa wa utunzaji wa mazingira ili kulinda sayari hii huku wakihakikisha riziki endelevu kwa vizazi vijavyo.

Katika masuala ya uvumbuzi kiongozi wa nchi alisema Kenya hivi maajuzi ilizindua kituo cha kwanza cha kidijitali cha uvumbuzi usiochafua mazingira kama njia ya kuchochea mawazo mapya ya uvumbuzi na bidhaa.

Alishukuru Rwanda kwa kuandaa awamu za kwanza nne za kongamano la Youth Connekt. Awamu ya 6 ilianza Disemba 8, 2023 na itakamilika Disemba 12 katika ukumbi wa KICC jijini Nairobi.

Website |  + posts
Share This Article