Rais William Ruto anatarajiwa kuondoka nchini Jumapili jioni kuelekea nchini Korea Kusini kwa ziara rasmi ya kiserikali.
Ziara hiyo inalenga kukamilisha kutiwa saini kwa mikataba ya maendeleo iliyoafikiwa mwezi Novemba mwaka jana, alipozuru taifa hilo la bara Asia.
Baadhi ya maafikiano ya mwaka jana ilikuwa serikali ya Korea Kusini itoe shilingi bilioni 40 kwa sekta ya uchumi bunifu na mitambo ya kujenga mabwawa ya unyunyuziaji maji mashamba ya thamani ya shilingi bilioni 25 .
Kwenye ziara hiyo, Rais atakutana na mwenyeji wake Yoon Suk Yeol.