Rais William Ruto amewateua mabalozi 23 na wasaidizi watakaohudumu katika mataifa ya kigeni baada ya kuidhinishwa na bunge la kitaifa.
Mabalozi walioteuliwa ni pamoja na:-Fred Outa aliyetumwa mjini Cairo nchini Misri ,Prof. Anne Kisaka Nanguli atakayehudumu Dakar,Senegal,Timothy Kaluma Mcharo anayeelekea Algiers,Algeria,Christopher Andrew Lang’at aliyetumwa Abidjan, Cote d’Ivoire,Jessica Muthoni Gakinya atakayehudumu Rabat,Morocco,Halima Yussuf Mucheke anayeelekea The Hague,Uholanzi na David Kiplagat Kerich wa Washington DC,Marekani.
Wengine ni Everylyne Mwenda Karisa wa Havana, Cuba,Dkt.Peter Mutuku Mathuki wa Moscow,Urusi,Moi Lemoshira wa Tokyo, Japan,Kenneth Milimo Nganqa wa Abu Dhabi, UAE,General Jonah Mwanqi wa Tehran, Iran, na Abdi Aden Korio anayeelekea Muscat, Oman.
Mabalozi wasaidizi ni pamoja na :-Catherine Kirumba Karemu wa London,Uingereza,Joash Arthur Maangi wa Kampala,Uganda,Lilian Tomitom wa Lusaka, Zambia,Caroline Kamende Daudi wa Ottawa, Canada,
Peter Mbogo Njiru wa Islamabad,Pakistan.
Mabalozi wa kudumu ni pamoja na:-Gertrude N. Angote wa UNEP,Grace Atieno Okara wa United Nations HABITAT,Fancy Too wa Geneva, Switzerland na Ekitela Erastus Lokaale wa Umoja wa mataifa mjini New York, USA.