Rais William Ruto ametetea ziara zake za ughaibuni akisema kuwa zimezaa matunda.
Kwenye mahojiano na wanahabari kutoka ikulu ya Nairobi, Ruto amesema ziara zake zimehahikisha nchi hii itanufaika pakubwa akitaja mfano wa ziara yake nchini China na Marekani.
Amekanusha madai ya kuwepo kwa matumizi mabaya ya pesa za serikali kwenye ziara hizo.
Rais ameweka bayana kuwa Kenya itanufaika pakubwa na miradi itakayoanza kutekelezwa humu nchini baada ya kutia saini mikataba na nchi za Marekani na China.