Ruto akutana na viongozi wa mashinani kutoka Kiambu Ikuluni Nairobi

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto amekutana na viongozi wa mashinani kutoka kaunti ya Kiambu katika Ikulu ya Nairobi na kuahidi kukamilisha miradi ya maendeleo iliyoanzishwa na serikali eneo hilo.

Alitaja baadhi ya miradi iliyotekelezwa katika kaunti ya Kiambu kama ujenzi wa masoko mapya 30 ua kisasa kwa gharama ya shilingi bilioni 4.5,na nyumba za gharama nafuu za kima cha shilingi bilioni 30.

Aidha Rais amesema serikali inajenga uwanja mpya wa michezo mjini Thika unaoselehi mashabiki 10,000 pamoja na ujenzi wa barabara ya umbali wa kilomita 240 ya Mau Mau na Muthaiga-Ndumberi kwa gharama ya shilingi bilioni 22.

Share This Article