Ruto akutana na Rais wa CAF Dkt. Motsepe kutathmini matayarisho ya fainali za CHAN

Dismas Otuke
1 Min Read
Rais Ruto akiwa na Rais wa CAF Dkt. Patrice Motsepe katika Ikulu ya Nairobi

Rais William Ruto amefanya kikao leo na maafisa wa kutoka Shirikisho la Soka barani Afrika, CAF wakiongozwa na kinara wake Dkt. Patrice Motsepe. Kikao hicho kilichofanyika katika Ikulu ya Nairobi kilijadili matayarisho ya Kenya kuandaa fainali za kombe la Afrika kwa wanasoka wa ligi ya nyumbani, CHAN mwezi Februari mwakani.

Ruto ametoa hakikisho la kujitolea kwa serikali kuhakikisha miundombinu imekamilika kwa wakati ufaao ili Kenya iandae fainali za CHAN.

Motsepe kwa upande wake amemshukuru Rais Ruto kwa jitihada za serikali yake kwa kudhihirisha kuwa na uwezo wa kuandaa mashindano ya kimataifa.

Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Waziri wa Michezo anayeondoka Kipchumba Murkomen  na viongozi wa soka nchini wakiongozwa na kinara wa FKF Hussein Mohammed.

Kenya itaandaa mechi za fainali za CHAN katika viwanja vya Kasarani na Nyayo ambayo kwa sasa vinakarabatiwa, huku Ulinzi Sports Complex , Police Sacco na Kirigiti Stadium katika kaunti ya Kiambu vikitumika kwa mazoezi ya timu zitakazoshiriki CHAN.

Kenya itaandaa fainali za CHAN kati ya Februari 1 na 28 mwaka ujao kwa ushirikiano na Tanzania na Uganda na kisha mataifa hayo yaandae kipute cha AFCON mwaka 2027.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *