Ruto akutana na Biden katika ikulu ya White House

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto alifanya mazungumzo na mwenzake wa Marekani Joe Bidden kwenye ikuli ya White House nchini Marekani Jumatano usiku.

Ulikuwa mkutano wa kwanza wa Rais Ruto na Biden katika ziara yake punde baada ya kuwasili kutoka jimbo la Atlanta.

Kwenye kikao hicho Marais hao wawili walizungumzia maswala ya teknolojia kwa kirefu,huku Ruto akimshukuru Rais Biden kwa kuwekeza kiwango kikubwa cha pesa katika miradi ya kiteknolojia humu nchini.

Ruto aliongeza kuwa ushirikiano wa Marekani na Kenya katika teknlojia utaimarisha fursa na kuboresha maisha sio tu ya Wakenya bali Afrika kwa ujumla.

Ruto ambaye yuko Marekani kwa ziara rasmi ya siku nne pia alikutana na Spika wa Bunge la waakilishi Mike Johnson, ambapo pia alijadiliana na Maseneta kadhaa wakiwemo wa chama cha Democrat na Republican.

 

Share This Article