Ruto akariri kuunga mkono ugatuzi

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto amesema serikali yake itaendelea kuunga mkono ugatuzi ambao ni kiungo muhimu cha mfumo wa kiuchumi wa kutokea chini kwenda juu almaarufu Bottom Up, katika juhudi za kueneza maendeleo mashinani.

Ruto amesema haya Jumatatu katika ikulu ya Nairobi alipoongoza kongamano la kumi la kitaifa lililoleta pamoja maafisa wa kaunti na wale wa serikali kuu.

Amesema kuwa tayari serikali yake kupitia kwa Hazina Kuu imetoa mgao wote wa pesa kwa serikali za kaunti katika mwaka wa fedha wa 2022/2023.

Pia amekariri kujitolea kuhakikisha huduma zote za ugatuzi ambazo zimesalia katika serikali kuu zimehamishiwa serikali za kaunti.

Ili kuafikia hilo, Ruto amesema jopo maalum limebuniwa kutathmini majukumu ya ugatuzi yaliyosalia katika serika kuu, ili kubuni mbinu mwafaka ya utoaji huduma.

Share This Article