Rais William Ruto amekariri kujitolea kwa serikali ya Kenya kuboresha mazingira ya michezo kwa wakimbizi nchini kupitia ujenzi wa miundo msingi na vifaa vya michezo .
Rais amesema serikali itashirikiana na tume ya umoja wa mataifa kuhusu wakimbizi (UNHCR), akidokeza uwezekano wa ujenzi wa kambi ya wanariadha eneo la Kakuma kaunti ya Turkana, ili kukuza vipaji vya wakimbizi michezoni.
Ruto amesema haya Ijumaa alipokutana na Rais wa kamati ya kimatifa ya Olimpiki IOC Thomas Bach katika ikulu ya Nairobi.
Bach ambaye yuko nchini kwa ziara rasmi ya siku tatu amekutana pia na wanariadha huko Eldoret na atakamilisha ziara yake kwa kukutana na wanamichezo wakimbizi mjini Turkana.