Rais William Ruto ni miongoni mwa viongozi wanaohudhuria uapisho wa Rais Hakainde Hichilema wa Zambia kwa muhula wa pili afisini.
Viongozi wengine wanaohudhuria uapisho huo ni Marais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe, Netumbo Nandi-Ndaitwah wa Namibia Samia Suluhu wa Tanzania miongoni mwa wengine.
Hafla ya kumuapisha Rais Hichilema inafanyika katika Uwanja wa National Heroes mjini Lusaka.
Tume ya Uchaguzi nchini Zambia ilimtamgaza Hichilema kuwa mshindi wa matokeo ya urais katika uchaguzi mkuu wa mwezi jana.
Hii ni baada ya kupata asilimia 60 ya kura zote zilizopigwa.
Waliokuwepo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, JKIA kumuaga Rais ni pamoja na Naibu wake Kithure Kindiki, Mkuu wa Majeshi Charlse Kahariri, Inspekta Mkuu wa Polisi Douglas Kanja na Katibu katika Wizara ya Usalama wa Kitaifa Dkt. Raymond Omollo.
Hakainde aliye na umri wa miaka 64 anakula kiapo kuhudumu kwa kipindi cha pili na cha mwisho cha miaka mitano.