Ruto ahudhuria mkutano mkuu wa kisiasa wa Umoja wa Mataifa

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto siku ya Jumatatu amehudhuria mkutano mkuu wa kisiasa katika kikao cha Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo endelevu mjini New York, Marekani.

Ruto pia alipata fursa ya kufanya mazungumzo na mwenzake wa Albania Bajram Begaj, aliyeelezea azma ya taifa lake kufungua ubalozi nchini Kenya.

Wakati huo huo rais Ruto alikutana na kiongozi wa Slovakia Zuzana Caputova, aliyeahidi kuisaidia Kenya katika mpango wa utengenezaji wa magari ya umeme kwa kutumia teknolojia ya kutengeneza betri za kisasa za umeme.

Rais William Ruto akiwa na Rais wa Slovakia Zuzana Caputova

Aidha Marais hao wawili waliafikiana kuboresha viwanda vya kutengeneza mbolea nchini Kenya na kuimarisha mbinu za usalama mitandaoni.

Share This Article