Ruto ahimiza watoaji mikopo kwa Afrika kujumuisha hela za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto amehmiza jamii ya kimataifa kutenga kiwango  cha pesa za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika mikopo wanayotoa.

Ruto alisema haya Jumatano alipohutubia kikao cha 59 cha benki ya maendeleo barani Afrika ,AfDB katika ukumbi wa mikutano ya kimataifa KICC, huku benki hiyo ikiadhimisha miaka 60 tangu ianzishwe.

Ruto ameongeza kuwa bara hii  limekabiliwa na changamoto kadhaa katika kipindi cha miaka 6 liyopita zikiwemo mabadiliko ya hali ya hewa yasiyotabirika.

Kulingana na Ruto ipo haja  ya jamii ya kimataifa  kujumuisha kiasi fulani cha pesa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Marais Paul Kagame wa Rwanda,Emerson Mnangagwa wa Zambia,Rasi wa Muungano wa Afrika-AU Mahamat Faki na Rais wa benki ya Maendeleo barani Afrika -AfDB  Adesina Akinwumi.

Kikao hicho kinatarajiwa kukamilika  tarehe 31 mwezi huu.

 

TAGGED:
Share This Article