Rais William Ruto amefungua miradi kadhaa ya maendeleo katika kaunti ya Nyamira katika siku ya kwanza ya ziara yake kwenye kaunti hiyo.
Akiwa Nyamira siku ya Jumatatu Ruto ametangaza ujenzi wa nyumba za gharama nafuu kwa kima cha shilingi bilioni 15 ,ujenzi wa soko la kisasa la shilingi milioni 70 huko Ikonge .
Aidha,Rais ametangaza kutengwa kwa shilingi milioni 900 kwa ujenzi wa uwanja wa michezo wa Nyamira na shilingi nyingine bilioni 1 kwa uboreshaji wa hospitali ya ya rufaa ya kaunti ya Nyamira.
Miradi mingine iliyokaguliwa na Rais ni pamoja na ujenzi wa barabara ya kilomita 61 ya Eronge–Kebuse hadi Omonyenya, iliyofikia asilimia 58 na ile ya Manga–Motemomwamu iliyo asilimia 38.
Rais yuko kwa ziara ya siku nne katika eneo la Kisii.