Ruto afungua jengo la Bunge Tower

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto mapema Alhamisi amefungua rasmi jengo la Bunge Tower lenye orofa 28, ambalo yatakuwa makao mapya ya afisi za wabunge wa mabunge yote mawili.

Jumba hilo la kisasa awali lilikuwa litumike na wabunge 320 wa bunge la kitaifa litatumika pia na maseneta 69 na limegharimu mabilioni ya pesa huku ujenzi wake ukidumu kwa zaidi ya mwongo mmoja.

Jengo la Bunge Tower

Ujenzi wa jengoi hilo ulianza mwaka 2010 na limegahrimu kima cha shilingi bilioni 9.6.

Rais Ruto aliandamana na naibu wake Rigathi Gachagua na alikaribishwa na Maspika wa mabunge yote mawili Moses Wetang’ula na Amason Kingi alipowasili.

Baadaye Rais aliwahutubia wabunge na maseneta kwenye kikao cha pamoja.

Website |  + posts
Share This Article