Rais William Ruto alifanya ziara ya ghafla nchini Haiti jana kutathmini mchakato wa maafisa wa polisi wa Kenya wanaolinda usalama.
Ruto alikutana na polisi wa Kenya wanaoshika doria katika mji mkuu wa Port -au Prince na kuwapongeza kwa kutekeleza vyema kazi yao kwa kushirikiana na polisi wa Haiti.
Kenya ilutuma polisi 400 nchini Haiti ujumbe wa kwanza wa maafisa 200, ukiwasili juni 25, na ule wa pili wa polisi 200 Julai 16 mwaka huu.
Muda wa kuhudumu kwa polisi wa Kenya na wengine kutoka nchi jirani za Belize na Jamaica, unatarajiwa kukamilika mwezi ujao lakini huenda Umoja wamataifa ukaongeza kipindi hicho.
Ruto aliwasili Ijumaa usiku mjini Newyork Marekani, kuhudhuria mkutano mkuu wa baraza la Umoja wa mataifa (UNGA) wiki hii.