RS Berkane waibwaga Zamalek fainali ya kombe la shirikisho

Dismas Otuke
1 Min Read

Klabu ya RS Berkane ya Morocco ikiwa nyumbani ilisajili ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya miamba wa Misri,Zamalek katika duru ya kwanza ya fainali ya kombe la shirikisho iliyosakatwa Jumapili usiku katika uchanjaa wa manispaa wa Berkane.

Nahodha Issoufou Dayo na Adil Tahif walipachika magoli katika kipindi cha kwanza kwa mabingwa hao mara mbili wakihitaji sare yoyote katika mkumbo wa pili ili kutwaa kombe hilo .

Ahmed Sayed,alitoa pasi kwa Seifeddine Jaziri mwanzoni mwa kipindi cha pili,huku akikomboa goli moja kwa Zamalek.

Marudio ya fainali hiyo ni Jumapili ijayo Mei 19 mjini Cairo huku mabingwa wakituzwa dolamilioni 1.5.

Website |  + posts
Share This Article