RS Berkana ya Morocco yapewa ushindi wa ubwete dhidi ya USM Alger ya Algeria

Dismas Otuke
1 Min Read

Klabu ya Morocco RS Berkane imepewa ushindi wa ubwete wa mabao matatu kwa bila dhidi ya wenyeji na mabingwa watetezi USM Alger ya Algeria katika duru ya kwanza ya nusu fainali kombe la shirikisho.

Mechi hiyo iliyoratibiwa kusakatwa Jumapili iliyopita ,lakini haikuchezwa baada ya wenyeji USMA kupinga uamuzi wa CAF wa kutowaadhibu wapinzani wao Berkane kutokana na sare waliyokuwa wamevalia.

Kamati inayosimamia mashindano ya vilabu SAfrika ilikutana Jumatano na kutoa uamuzi wa kuwapa Berkane ushindi wa ubwete wa mabao matatu kwa bila katika mchuano huo, huku marudio yakipangiwa Jumapili hii Aprili 28 katika uwanja wa Berkane Municipal nchini  Morocco.

Kamati hiyo pia imewasilisha kesi hiyo kwa jopo la nidhamu ili Berkane wachukuliwe hatua zaidi za kinidhamu.

Kufuatia uamuzi huo Berkane wanakaribia kufuzu kwa fainali ya kombe hilo wanalowinda kwa mara ya tatu ,wakati USMA wakiwa na kibarua cha kugeuza mechi hiyo wakilazimika kushinda kwa magoli manne kwa bila ili kufuzu wa fainali .

Share This Article