Katibu wa Wizara ya Kilimo Kipronoh Rono siku ya Jumatatu alikagua shughuli inayoendelea ya usambazaji mbolea katika ghala kadhaa za Halmashauri ya Nafaka na Mazao nchini – NCPB maeneo ya North Rift na magharibi mwa nchi.
Ronoh alizuru vituo vya NCPB vya Kitale, kampuni ya Kenya Seed kaunti ya Trans Nzoia, ghala za NCPB za Eldoret kaunti ya Uasin Gishu na Moi’s Bridge kaunti ya Trans Nzoia.
Katibu huyo ataongoza shughuli ya usambazaji mbolea ya bei nafuu kwa wakulima kote nchini katika juhudi za kuimarisha kilimo.
Amesema kuwa magunia ya mbolea 130,000 yatagawiwa wakulima kote nchini katika msimu wa sasa wa upanzi.
Ronoh aliandamana na Mbunge wa Kwanza Ferdinand Wanyonyi na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kenya Seed Sammy K. Chepsiror na viongozi wengine.