Rodri ateuliwa kuwania tuzo ya mwanandinga bora wa mwaka ya FIFA

FIFA BEST

Dismas Otuke
2 Min Read

Kiungo wa Manchester City na Uhispania Rodri,ameteuliwa kuwania tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka huu katika tuzo za shirikisho la kandanda Ulimwenguni FIFA.

Rodri alitwaa tuzo ya Ballon D’or kwa mara ya kwanza mwezi mmoja uliopita, baada ya kutamba msimu uliopita akiwa na Uhispania na pia Mancity.

FIFA imetoa orodha ya wachezaji 11 ,makocha na vilabu  kuwania tuzo bora za mwaka huu maarufu kama FIFA BEST.

Mashabiki watawapigia kura wachezaji ,makocha na vilabu huku siku ya mwisho ya kupiga kura ikiwa Disemba 10 mwaka huu.

Tuzo za mwaka huu zinajumuisha vitengo vya mchezaji bora wa mwaka kwa wanaume na wanawake,Kipa bora,kocha bora wa mwaka kwa wanaume na wanawake na bao bora la mwaka.

Waaniaji wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kwa wanaume ni pamoja na:-Dani Carvajal (Spain), Real Madrid,Erling Haaland (Norway), Manchester City,Federico Valverde (Uruguay), Real Madrid,Florian Wirtz (Germany), Bayer Leverkusen,Jude Bellingham (England), Real Madrid,Kylian Mbappé (France), Paris Saint-Germain/Real Madrid,Lamine Yamal (Spain), Barcelona,Lionel Messi (Argentina), Inter Miami,Rodri (Spain), Manchester City,Toni Kroos (Germany), Real Madrid (now retired) na Vinícius Jr (Brazil), Real Madrid.

Tuzo ya kocha bora wa mwaka inawaniwa na:-Carlo Ancelotti (Italy), Real Madrid,Lionel Scaloni (Argentina), Argentina,Luis de la Fuente (Spain), Spain,Pep Guardiola (Spain), Manchester City na Xabi Alonso (Spain), Bayer Leverkusen.

Wanandinga saba walio kwenye orodha ya kuwania tuzo ya kipa bora kwa wanaume ni:-Andriy Lunin (Ukraine), Real Madrid,David Raya (Spain), Arsenal,Ederson (Brazil), Manchester City,Emiliano Martínez (Argentina), Aston Villa
Gianluigi Donnarumma (Italy), Paris Saint-Germain,Mike Maignan (France), AC Milan na Unai Simón (Spain), Athletic Club.

Hafla hiyo itaandaliwa mapema mwaka ujao.

Lionell Messi wa Argentina na klabu ya Inter Miami pamoja na Aitana Bonmatti wa Uhispania walituzwa washindi wa makala ya mwaka jana.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *