Rising Lionesses yawasili Kenya baada ya kunyakua dhahabu Dakar

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Kenya ya raga kwa wasichana chipukizi saba kila upande almaarufu Rising Lionesses,  imewasili nchini mapema Ijumaa kutoka Dakar,Senegal ilikonyakua dhahabu katika Olimpiki ya chipukizi.

Vidosho hao wa Kenya waliibwaga Australia pointi 17-12 katika muda wa ziada kwenye fainali ya kukata na shoka na kushinda dhahabu ya kwanza kwa Kenya katika makala ya nne ya Olimpiki ya chipukizi yanayoandaliwa kwa mara ya kwanza barani Afrika.

Timu hiyo ilipokelewa na Mkurugenzi wa michezo Douglas Ratemo punde ilipowasili.

 

 

Share This Article