Ripoti ya EACC: West Pokot kidedea katika utoaji rushwa

Martin Mwanje
1 Min Read

Kaunti ya West Pokot ilikumbwa na visa vingi vya ulipaji rushwa mwaka wa 2023. 

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na EACC leo Jumatano juu ya Utafiti wa Maadili ya Kitaifa na Ufisadi 2023, washiriki walisema walilipa kitita kikubwa cha rushwa katika kaunti hiyo kikiwa shilingi 56, 695.

Kaunti ya Nairobi iliorodheshwa ya pili katika visa vya utoaji rushwa huku waliohojiwa wakisema walilipa shilingi 37,768, Murang’a 18,378, Kisii 16,810 huku rushwa ya shilingi 11,136 ikilipwa katika kaunti ya Uasin Gishu.

Katika kaunti ya Kitui, rushwa ya shilingi 9,849 ilitolewa, Busia 7,468 na Tharaka Nithi waliohojiwa wakishtakia kulipa rushwa ya shilingi 7,041.

Kwa mujibu wa utafiti huo, kiwango kikubwa cha mgao wa rushwa kitaifa kililipwa katika kaunti ya Nairobi kikiwa asilimia 54.45 ikifuatwa na kaunti ya West Pokot kwa silimia 13.8 na kaunti ya Uasin Gishu asilimia 3.7.

Kwa kuangazia taasisi za umma zinazopokea hongo, Mamlaka ya Uchukuzi na Usalama Barabarani, NTSA iliongoza katika visa vya upokeaji hongo kitaifa kwa asilimia 33.6 ikifuatwa na polisi kwa asilimia 20.7 na polisi wa trafiki kwa asilimia 3.7.

Share This Article