Rickman Manrick aibuka mshindi wa pigano la ndondi dhidi ya Grenade

Pigano hilo lilipangwa na ligi ya mabingwa wa ndoni nchini Uganda, ili kumaliza ugomvi kati ya wawili hao.

Marion Bosire
1 Min Read
Grenade Official na Rickman

Mwanamuziki wa Uganda Rickman Manrick aliibuka mshindi katika pigano la ndondi dhidi ya mwanamuziki mwenza Grenade Official.

Pigano hilo lilipangwa na ligi ya mabingwa wa ndoni nchini Uganda, ili kumaliza ugomvi kati ya wawili hao.

Ugomvi huo ulifahamika kwa mara ya kwanza mwaka 2023 wakati waligombana katika eneo la burudani la ‘La Terezza’ jijini Kampala.

Grenade ndiye alianzisha ugomvi kwa sababu alikuwa bado ana hisia kwa mpenzi wake wa zamani mwanamuziki Sheila Gashumba aliyekuwa katika eneo hilo na mpenzi wake Rickman Manrick.

Wanaume hao walipigana siku hiyo kiasi kwamba Rickman aliumizwa mdomo huku Grenade akilazimika kujificha kwa muda asikamatwe na polisi.

Waliwahi kukutana tena kwenye studio za kituo cha redio cha Galaxy FM ambapo Rickman alisema alikuwa na kinyongo na Grenade.

Alikosa kumsalimia na kufafanua kwamba alikuwa na shida naye kama mtu na wala sio muziki wake, ambapo pia alisema anapenda muziki wake.

Hapo ndipo wazo la pigano la ndondi lilitolewa na Rickman akalikubali huku Grenade akisema angefikiria kwanza.

Mwezi Mei mwaka huu, Gashumba alitangaza kwamba uhusiano wake wa kimapenzi na Rickman umefikia kikomo akielezea kwamba waliafikiana kuumaliza.

Inasubiriwa kuona iwapo wanaume hao wawili hao watazika tofauti zao katika kaburi la sahau.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *