Shirikisho la Riadha Ulimwenguni limerasmisha rekodi ya dunia ya kilomita 5 inayoshikiliwa na bingwa wa Olimpiki Beatrice Chebet.
Chebet alishinda mbio za nyika za Cursa Dels Nassos mjini Barcelona Disemba 31 mwaka jana kwa muda wa dakika 13 na sekunde 54, akivunja rekodi ya awali kwa sekunde 19,na kuwa mwanamke wa kwanza kutimka mbio hizo chini ya muda wa dakika 14.
Chebet aidha, anashikilia rekodi ya dunia ya mita 10,000 aliyosajili katika mbio za Preontaine Classic mwaka jana nchini Marekani.