Iwapo ataidhinishwa na bunge, basi Rebecca Miano ataandikisha historia kwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa kwanza mwanamke.
Siku ya Ijumaa akitaja nusu ya kwanza ya mawaziri 11, Rais William Ruto alimteua Rebecca Miano ambaye awali alikuwa waziri wa biashara na viwanda, kuwa Mwanasheria Mkuu.
Anatarajiwa kuchukua wadhifa ulioshikiliwa na Justin Muturi, ambaye alitimuliwa katika Baraza la Mawaziri la awali.
Kabla ya kujiunga na Baraza la Mawaziri, Miano alihudumu wadhifa wa Mkurugenzi Mkuu wa shirika la KENGEN.
Miano ana shahada ya digrii katika maswala ya sheria na shahada ya post graduate katika somo la comparative Law.
Wizara alzoshikilia awali ni pamoja na ile ya Jumuiya ya Afrika mashariki, maeneo kame na ustawi wa kimaeneo na wizara ya biashara na viwanda.
Wadhifa wa mwanasheria mkuu umewahi kushikiliwa na Charles Njonjo, James Karugu, Joseph Kamere, Matthew Guy Muli, Amos Wako, Prof. Githu Muigai, Justice Kihara Kariuki na Justin Muturi.