Klabu ya Real Valladolid inayomilikiwa na mshambulizi wa zamani wa Brazil Ronaldo, imefuzu kushiriki Ligi Kuu nchini Uhispania -La Liga, baada ya kuenguliwa msimu uliopita .
Valladolid inalipandishwa ngazi Jumapili baada ya kusajili ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Villarreal B,wakiongoza jedwali kwa alama 72 ikisalia mechi moja msimu ukamilike.
Leganes waliotoka sare watalazimika kutoka sare katika mchuano wa mwisho watakapowaalika Elche Juni 2 ili kurejea tena ligi kuu.