Razack Adamu mshindi wa BSS awamu ya 14

Marion Bosire
1 Min Read

Razack Adamu ndiye mshindi wa awamu ya 14 ya Bongo Star Search – BSS nchini Tanzania. Raia huyo wa mkoa wa Arusha alitangazwa kwenye fainali iliyofanyika katika ukumbi wa Warehouse Arena, Masaki, Dar es Salaam.

Yeye ndio wa kwanza kutoka mkoa wa Arusha kuwahi kuibuka mshindi wa BSS.

Aliwapiku wenzake King David kutoka Mwanza, Eva, Allan na Frank wote wa Dar es Salaam, na kunyakua zawadi ya pesa milioni 30 za Tanania pamoja na shamba.

Mshindani mmoja kwa jina Lidya kutoka Arusha ndiye nambari 6 kwa mashindano hayo na aliondolewa mapema jana.

Allan Mwijage wa Dar es Salaam alipatiwa tuzo ya mwaniaji maarufu zaidi kwenye shindano hilo la BSS lililoanza mwezi Septemba mwaka jana.

Mbunge Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA ambaye ni naibu waziri wa utamaduni sanaa na michezo ndiye alikuwa mgeni rasmi wa shughuli hiyo ambapo washindani 6 walikuwa wanang’ang’ania nafasi ya kwanza.

Mwinjuma alipongeza washiriki wote wa BSS huku akituza wa mwisho 6 shilingi laki 5 kila mmoja pesa za Tanzania.

Majaji wa awamu ya 14 ya BSS ni mwanzilishi wa BSS Madam Rita, mwanamuziki Shilole, watangazaji Meena Ali, Salama Jabir na Master Jay.

Share This Article