Raymond Omollo aridhishwa na maandalizi ya sherehe za Mashujaa

Tom Mathinji
1 Min Read
Katibu katika wizara ya Usalama Raymond Omollo akagua uwanja wa Kericho Green.

Katibu katika wizara ya usalama wa taifa Dkt. Raymond Omollo, amesema serikali imeridhishwa na ukarabati wa uwanja wa Kericho Green, utakaotumika kuandaa sherehe za Mashujaa za mwaka huu.

Dkt. Omollo aliyezuru uwanja huo kukagua shughuli za ukarabati, alisema ana imani kwamba kufikia tarehe 10 mwezi huu, ukarabati katika uwanja huo utakuwa umekamilika kwa asilimia 100.

Akiwahutubiwa wanahabari katika uwanja huo, katibu huyo alidokeza pia, barabara zinazoelekea katika uwanja huo zinakarabatiwa, kufanikisha usafiri kuingia na kuondoka katika uwanja huo.

Aidha Dkt. Omollo alisema mashujaa watatambuliwa wakati wa sherehe hizo, ambao walijitolea kukomboa taifa hili na mchango wao mkubwa wa kuhakikisha taifa hili linaafikia maendeleo.

Kulingana na Omollo wahamasishaji wa afya kutoka kote nchini watazinduliwa wakati wa sherehe hizo.

Akizungumza katika hafla hiyo, katibu katika wizara ya afya Mary Muthoni, alithibitisha kuwa kuwa rais William Ruto atawazindua wahamasishaji 100,000 wa afya wakati wa sherehe ya Mashujaa za mwaka huu, ambayo kauli mbiu yake ni , huduma ya afya kwa wote.

Alisema maafisa wa afya ya umma watakagua hoteli zote mjini Kericho, kuhakikisha ubora wa hali ya juu ya usafi.

Share This Article