Rangers watoka nyuma na kuwabwaga Homeboyz

Dismas Otuke
1 Min Read

Posta Rangers wametoka nyuma na kusajili ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kakamega Homeboyz katika mechiya kwanza ya raundi ya 31 kuwania ubingwa wa Ligi kuu Kenya, iliyosakatwa Jumamosi adhuhuri katika uwanja wa Police Sacco.

Brian Eshihanda aliwaweka wageni Homeboyz uongozini kunako dakika ya 10 ya mchezo na kungoza hadi mapumzikoni.

Mwinyi Shami Kibwana aliwarejesha wenyeji mchezo kwa goli la kusawazisha katika dakika ya 55 kupitia mkwaju wa penati, kabla ya kiungo Felix Oluoch, kupachika bao la ushindi dakika 13 baadaye.

Ushindi huo umewachupisha Rangers hadi nafasi ya saba kwa alama 46,pointi mbili zaidi ya Homeboyz zikisalia mechi tatu msimu ukamilike.

Website |  + posts
Share This Article