Rais Cyril Ramaphosa amehudhuria mazishi ya Balozi wake nchini Ufaransa Nathi Mthethwa siku ya Jumapili katika eneo la KwaMbonambi, KwaZulu-Natal.
Balozi Nathi alijitoa uhai baada ya kujirusha kutoka orofa ya 22 ya jengo moja jijini Paris.
Mazishi hayo yameandaliwa siku chache baada ya maafisa wa ujasusi wa Afrika na wale wa Ufaransa waliokuwa wakifanya uchunguzi wa kifo cha Balozi huyo kuondoa mbali uwezekano wake kuuawa.