Rais Zelensky kukutana na Chansela wa Ujerumani Ijumaa

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky (Kushoto), kukutana na Chansela wa Ujerumani Ijumaa.

Chansela wa Ujerumani Olaf Scholz na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, watashiriki mazungumzo Ijumaa Jijini Frankfurt, haya ni kulingana msemaji wa serikali ya Ujerumani.

Mkutano huo wa ana kwa ana, unajiri huku majeshi  ya kigeni yanayounga mkono Ukraine, Marekani ikiwemo, yakikutana katika kambi moja ya jeshi la wanahewa nchini Ujerumani, kupanga mikakati ya kuisaidia Kyiv.

Msemaji huyo aidha hakutoa habari zaidi kuhusu ziara ya Zelensky nchini Ujerumani, lakini duru zinasema kuwa atahudhuria mkutano huo katika kambi ya jeshi la wanahewa la Ramstein, Kusini Magharibi mwa Frankfurt.

Uwepo wa Zelensky, unalenga kuonyesha hali halisi ilivyo nchini Ukraine, siku chache baada ya watu 55 kufariki na wengine 300 kujeruhiwa kufuatia mashambulizi ya angani ya Urusi katika mji wa Poltava.

Mkuu wa majeshi wa Marekani Lloyd Austin, ataongoza mkutano huo.
Share This Article