Rais William Ruto ahudhuria ibada Meru

Marion Bosire
1 Min Read
Rais William Ruto katika kaunti ya Homa Bay.

Rais William Ruto kwa sasa anahudhuria ibada ya Jumapili huko Laare, eneo bunge la Igembe kaskazini kaunti ya Meru.

Kiongozi wa nchi ameandamana na viongozi wengi wa eneo hilo kwa ibada hiyo ya dini na madhehebu mbali mbali akiwemo gavana wa kaunti ya Meru Kawira Mwangaza.

Wengine ni waziri wa kilimo Mithika Linturi na seneta wa kaunti ya Meru aliyepia naibu spika wa bunge la seneti Murungi Kathuri.

Jana kiongozi wa nchi alizuru kaunti ya Nyeri ambapo alifungua afisi za chama cha UDA kati ya shuguli nyingine nyingi.

Share This Article