Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter afariki

Martin Mwanje
1 Min Read
Jimmy Carter - Rais wa zamani wa Marekani ambaye amefariki

Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 100.

Carter aliapishwa kuchukua madaraka kama Rais wa Marekani Januari 20, 1977.

Wakati wa uongozi wake, alikabiliana na kipindi cha miaka minne iliyokumbwa misukosuko ikiwa ni pamoja na kupanda kwa mfumko wa bei na ongezeko la ukosefu wa ajira.

Carter alilimbikiziwa mno sifa kutokana na sera zake za mambo ya nje.

Alianzisha kituo kilichojulikana kama Carter Centre.

Kama mkuu wa kituo hicho, Carter alisafiri zaidi ya maaifa 80 kufuatilia chaguzi zilizokumbwa na matatizo, kuwa mpatanishi wa mizozo mbalimbali na kupambana na magonjwa miongoni mwa harakati zingine.

Ni harakati ambazo zilikuwa chanzo cha yeye  kushinda Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 2002.

“Naiangalia kazi ninayoifanya kwenye Carter Center kama muendelezo wa kile ambacho nilijaribu kama rais. Unajua, tumeleta amani kati ya Israel na Misri. Tulifungua uhusiano mkubwa sana na Latin Amerika kwa mkataba wa Mfereji wa Panama,” alisema.

“Kwa hiyo kile ambacho nimekifanya tangu wakati huo imekuwa ni muendelezo.

 

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *