Rais wa zamani wa Gabon,Bongo na wanawawe wasusia chakula

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais wa zamani wa Gabon Ali Bongo na wanawe wa kiume wawili ,Jalil na Bilal,wameanza kususia chakula kupinga kuteswa kwa familia yao na kutengenanishwa.

Mawakili wa Rais huyo wa zamani Francois Zimeray na Catalina de la Sota, wamewasilisha kesi katika mahakama ya Paris nchini Ufaransa wakiitaka ichunguze madai hayo dhidi ya Bongo anayepanga kuzuru Paris hivi karibuni.

Bongo aling’atuliwa mamlakani Agosti mwaka 2023 na Mkuu wa majeshi Brice Oligui Nguema, na wamekuwa kwenye kifungo cha nyumbani tangu wakati huo.

Kulingana na mawakili,Sylvia Bongo mkewe Bongo alipigwa na kulazimishwa kushuhudia wanawake wa kiume Noureddin, Jalil na Bilal wakipigwa na kuteswa mara kadhaa.

Share This Article