Rais wa zamani wa Algeria Liamine Zeroual afariki

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali ya Algeria imetangaza maombolezo ya kitaifa ya siku tatu kufuatia kifo cha Rais wa zamani wa nchi hiyo Liamine Zeroual siku ya Jumapili. 

Zeroual alifariki akiwa na umri wa miaka 84.

Mwanajeshi huyo wa zamani alikuwa Rais nchini Algeria baina ya mwaka 1994 na 1999.

Hata hivyo, mwaka 1998, Zeroual alikatiza uongozi wake wa miaka mitano na kumwachia madaraka Abdelaziz Bouteflika ambaye aliongoza nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 20.

Share This Article