Rais wa Ureno avunja bunge, aitisha uchaguzi mwezi Machi mwakani

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais wa Ureno Marcelo Rebelo de Sousa amevunjilia mbali bunge la taifa hilo na kuitisha uchaguzi mdogo mwezi Machi mwaka ujao.

Hatua hii inajiri siku mbili pekee baada ya Waziri Mkuu kujiuzulu kutokana na tuhuma za ufisadi na uchunguzi unaoendelea dhidi yake.

Rebelo de Sousa alisema jana Alhamisi kuwa uchaguzi mdogo utaandaliwa Machi 10 mwaka ujao.

Waziri Mkuu Antonio Costa alijiuzulu Jumanne wiki hii kufuatia kukamatwa kwa msimamizi wake mkuu ikiwa sehemu ya uchunguzi unaoendelea kutokana na tuhuma za ufisadi.

Costa aliye na umri wa miaka 62 aliingia mamlakani mwaka 2015.

Amekanusha kutekeleza uovu wowote lakini hataendelea na majukumu yake.

Website |  + posts
Share This Article