Rais wa Ujerumani aomba Watanzania msamaha kwa maovu ya wakati wa ukoloni

Marion Bosire
1 Min Read
Rais Steinmeier akihutubia mkutano katika Ikulu ya Rais nchini Tanzania

Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier anayezuru Tanzania, ameomba radhi raia wa nchi hiyo ya Afrika Kusini kwa maovu ambayo nchi yake ilitekeleza nchini humo wakati wa ukoloni.

Wanajeshi wa Ujerumani waliua watu wapatao laki 3 nchini Tanzania wakati wa maasi ya Maji Maji mwanzo wa miaka ya 1900s, mojawapo ya maasi mabaya zaidi dhidi ya ukoloni.

Rais Steinmeier alikuwa akizungumza kwenye makavazi huko Songea ambapo maasi ya maji maji yalianzia.

Anatumai kwamba Tanzania na Ujerumani zitashirikiana katika mchakato wa pamoja wa kugusia mambo ya jadi.

Mafuvu ya vichwa vya baadhi ya viongozi wa maasi ya Maji Maji yalichukuliwa nchini Ujerumani kuonyeshwa kwenye makavazi.

Jamaa zao wamekuwa wakitafuta kurejeshwa kwa mafuvu hayo nchini Tanzania na tayari yametambuliwa kupitia vipimo vya msimbojeni almaarufu DNA.

Steinmeier alizungumza kuhusu suala la kurejeshwa kwa mabaki ya miili ya watu hao na akaahidi kwamba Ujerumani itashirikiana na Tanzania katika kile alichokitaja kuwa urejesho wa mali ya kitamaduni.

Msamaha huo wa Ujerumani umejiri baada ya Mfalme Charles wa tatu wa Uingereza kukiri kuhusu vitendo vya kikatili dhidi ya wakenya walipokuwa wakipambania uhuru.

Aliyasema hayo jijini Nairobi.

Website |  + posts
Share This Article