Rais wa Soka nchini Nigeria ajiuzulu

Wanachama hao wanane kati ya 13 wa bodi hiyo waliojiuzulu wanafanya maafisa watano waliosalia kutokuwa na uwezo wa kuendesha shule za kawaida za NFF.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais wa Shirikisho la Soka nchini Nigeria (NFF) Ibrahim Gusau amejiuzulu pamoja na wanachama wanane wa bodi hiyo kufuatia shinikizo kali kuhusu usimamizi duni.

Gusau ameshutumiwa kuhusiana na kukosa kufuzu kwa timu ya wanaume kwa Kombe la Dunia mwaka huu na pia kushindwa kufuzu kwa timu ya wanawake kwa Kombe la Dunia mwakani kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1991 katika historia ya nchi hiyo.

Wanachama hao wanane kati ya 13 wa bodi hiyo waliojiuzulu wanafanya maafisa watano waliosalia kutokuwa na uwezo wa kuendesha shule za kawaida za NFF.

Yamkini kumekuwa na uetepetevu wa hali ya juu katika uongozi wa soka nchini Nigeria huku wanachama wa bodi wakiwa na ushawishi kuhusu wachezaji wanaojumuishwa katika timu za taifa.

Share This Article